Dodoma FM

Wakazi wa Ihumwa waomba kituo cha treni ya SGR

30 October 2026, 16:58

Picha ni mwonekano wa Treni ya kisasa ya SGR. Picha na TRC.

Ombi hilo linatolewa wakati Ihumwa ikiendelea kuandaliwa kuwa eneo muhimu la shughuli za usafirishaji na usafirishaji wa mizigo. Eneo hilo lina zaidi ya ekari 5,000 zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa bandari kavu, huku pia kukiwa na eneo la matengenezo na usafi wa treni za SGR linalojulikana kama Ihumwa Marshalling Yard, Depot and Workshop.

Na Victor Chigwada.

Wakazi wa Kata ya Ihumwa jijini Dodoma wameiomba Serikali kuweka kituo kidogo cha kupakia na kushusha abiria wa treni ya mwendokasi ya SGR katika eneo hilo ili kurahisisha usafiri kwa wakazi wa Ihumwa na maeneo ya jirani.

Wakitoa ombi hilo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, wananchi hao wamesema kwa sasa abiria wanaotumia treni hiyo hulazimika kushukia Stesheni Kuu ya Mkonze na kutumia gharama nyingine za usafiri kufika Ihumwa, hali wanayoieleza kuwa usumbufu kwao.

Akijibu ombi hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amesema amepokea maombi ya wananchi hao, lakini ameeleza kuwa eneo hilo bado halina miundombinu ya barabara inayotosheleza mahitaji ya kituo hicho. Ameahidi kuwa baada ya TANROADS kukamilisha ujenzi wa barabara za kuingia na kutoka eneo hilo, atawasilisha ombi hilo kwa mamlaka na wasimamizi wa reli ya SGR kwa ajili ya kulifanyia kazi.

Simulizi na Victor Chigwada.