Dodoma FM

Hospitali ya wilaya Bahi kuanza kutoa huduma za watoto Njiti

17 April 2023, 2:45 pm

Jengo la huduma za dharura (EMD) hospitali ya Wilaya ya Bahi. Picha na Bernad Magawa.

Kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa halmashauri ya wilaya ya Bahi zaidi ya miaka kumi iliyopita, wananchi wameanza kupata huduma muhimu za afya ambazo walizifuata katika hospitali ya mkoa wa Dodoma lakini kwa sasa huduma zote zinapatikana wilayani Bahi.

Na Bernad Magawa .

Hospitali ya wilaya ya Bahi imeanza kutoa huduma za watoto wanaozaliwa kabla ya muda (Njiti) baada ya miundombinu ya majengo na vifaa tiba kukamilika.

Huduma hiyo muhimu ambayo hapo awali iliwalazimu wananchi kuifuata umbali wa zaidi ya kilomita 55 Katika hospitali ya mkoa imeelezwa kuokoa watoto wengi ambao wangeweza kupoteza maisha kwa kukosa huduma hiyo.

Akieleza kuhusiana na huduma hizo Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Bahi ambayo ni miongoni mwa hospitali mpya zilizojengwa na serikali hivi karibuni hapa nchini Dk. Kasimu kolowa amesema huduma zote muhimu za hadhi ya hospitali kwa sasa zinatolewa hospitalini hapo.  

Sauti ya Dr. Kasimu kolowa.

Katika hatua nyingine Dk. Kolowa ameeleza kuanza kutolewa kwa huduma za dharura (EMD) katika hospitali hiyo jengo lililojengwa na serikali kwa fedha za uviko 19 likigharimu million 300.