Dodoma FM

Wakazi wa Igungulile walazimika kutumia maji ya Mabwawa

21 January 2023, 10:13 am

Na; Victor Chigwada.                                                

Kukosekana kwa huduma ya Maji safi na salama imetajwa kuwa ni sababu ya Wananchi wa kijiji cha Igungulile wilayani Chamwino kutumia  maji ya mabwawa.

Mwenyekiti wa kijiji cha Igungulile Bw.Hamisi Msangi amesema changamoto ya maji imesababisha wananchi wake kutumia maji ambayo sio safi na salama.

Msangi amesema kuwa licha ya juhudi za serikali  kuchimba visima virefu lakini maji hayo yamekuwa na  wingi wa chumvi hali ambayo hayafai kutumiwa na binadamu.

Mwenyekiti huyo amesema njia mbadala itakayowezesha kutatua tatizo hilo ni serikali kuwasaidia kuunganisha mtandao wa bomba za maji kutoka kijiji jirani ili kuondokana na adha ya kutumia  maji ya mabwawani

Naye Diwani wa Kata ya loje Wilaya ya Chamwino Bw.John Njohoka amekiri licha ya chngamoto hiyo lakini wanaishukuru Serikali kwa msaada wa baadhi ya visima

Amesema baadhi ya visima vimegundulika  kuwa na maji  yenye chumvi kali ambayo hayafai kwa matumizi ya binadamu na kuiomba Serikali kuendelea na jitihada za kupeleka huduma.