Dodoma FM

Akinamama watakiwa kuzingatia muda wa kunyonyesha watoto

27 September 2023, 4:57 pm

Akina mama wametakiwa kuzingatia usafi kabla ya kumnyonyesha mtoto ili kuepukana na maambukizi mbalimbali. Picha na UN News.

Wataalamu wa Afya hushauri mtoto kunyonyeshwa maziwa ya mama kwa muda stahiki hasa kwa miezi sita ili kuijenga afya ya mtoto pamoja na kumpatia baadhi ya vyakula kwa ajili ya afya bora kwa mtoto.

Na Naima Chokela.          

Ni muhimu kuzingatia afya ya mtoto ikiwa ni kunyonyeshwa kwa muda unaotakiwa ili kumjenga vizuri katika ukuaji wake.

Mtaalamu katika malezi na makuzi ya awali ya mtoto Bw.Loata Mollel amesema hayo wakati akizungumza na Dodoma fm na kuwataka kina mama kuzingatia kuwanyonyesha watoto kwa muda wa miezi sita ili kuwa na afya njema.

Sauti ya Bw. Loato Mollel.
Picha ni mama akinyonyesha mtoto wake. Picha na UN News.

Aidha amewataka kina mama kuzingatia usafi kabla ya kumnyonyesha mtoto ili kuepukana na maambukizi mbalimbali, pia kuhudhuria kliniki mara kwa mara ili kuweza kupata msaada zaidi .

Sauti ya Bw. Loato Mollel.