Wananchi Handali walalamika kucheleweshewa fidia
8 July 2026, 17:44

Jitihada za kumpata mhandisi wa maji Wilaya ya Chamwino kujibu malalamiko haya bado zinaendelea
Na Victor Chigwada.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Handali walio hama makazi yao na kupisha mradi wa maji wamelalamika kucheleweshewa malipo ya fidia zao.
Wananchi hao walilazimika kupisha eneo hilo kwaajili ya mradi wa maji ambapo waliahidiwa kulipwa fidia lakini hadi sasa wanadai fidia hiyo imelipwa kwa wananchi wachache na baadhi yao walipata nusu ya malipo na wengine hawakupata kabisa malipo hayo.
Aidha walio lipwa fidia hiyo wanaedai pesa waliyo lipwa ni ndogo na haiwatoshi wao kwenda kuanzisha makazi sehemu nyingine.
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Handali Bw.Mashauli Machea amekiri kuwepo Kwa malalamiko hayo ya ucheleweshaji wa fidia ambapo amesema bado wanaendelea kufuatilia kwa Mamlaka husika RUWASA pamoja na kwa mkandarasi aliyepewa tenda hiyo.