Dodoma FM

Tanzania yaonyesha kuwa na idadi ndogo ya watu wanao tumia maziwa

21 July 2022, 1:52 pm

Na; Benard Filbert.

Imeelezwa kuwa licha ya uzalishaji wa maziwa kuongezeka nchini bado kuna changamoto kutokana na  idadi ndogo ya watu ambao wanatumia maziwa.

Hayo yameelezwa na Israel Mwingira afisa uzalishaji kutoka bodi ya maziwa Tanzania wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha The Morning Power ambacho kinaruka kupitia Dodoma Tv.

Bwana Israel amesema changamoto ya baadhi ya watu kutokunywa maziwa nikutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha ambapo hivi sasa wamekuja na mradi wakuhamasisha unywaji wa maziwa kuanzia shule za msingi.

.

Naye Radilan Hilal ambaye pia ni afisa uzalishaji kutoka bodi hiyo amesema hivi sasa wanao mpango wa kurasimisha bodi hiyo ili iweze kufanya majukumu yake ipasavyo na wiki ijayo wana mpango wakukutana na wauzaji wa maziwa ili kuwafundisha namna bora ya kuandaa maziwa.

.

Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wananchi kama wanatambua umuhimu wa kunywa maziwa ambapo wamekiri kutokuwa na elimu yakutosha na kujua umuhimu wa kunywa maziwa.

Bodi ya maziwa ni taasisi ya umma ipo chini ya wizara ya mifugo na uvuvi huku majukumu yake ikiwa kusimamia sekta ya maziwa nchini.