Dodoma FM

Belege waishukuru serikali kuboresha sekta ya Elimu

11 May 2022, 2:45 pm

Na; Victor Chigwada.

Wananchi wa Kata ya Belege Wilayani Mpwapwa wameishukuru Serikali ya awamu ya tano pamoja na awamu ya sita kwa jitihada za kuboresha sekta ya elimu

Akizungumza na taswira ya habari Diwani wa Kata hiyo kwa niaba ya wananchi Baraka Habari ameishukuru Serikali kwa kuwaongezea vyumba vya madarasa upande wa Serikali licha ya ukosefu wa maabara katika shule hiyo

.

Habari ameongeza kuwa katika Hali ya kukabiliana na changamoto hiyo ya maabara tayari wamepitisha   azimio la ujenzi wa vyumba viwili vya bailojia na kemia

.

Aidha Diwani wa Kata hiyo ameiomba Serikali kuwasidia changamoto ya nyumba za walimu pamoja na vyumba vya madarasa upande wa shule ya msingi

.

Serikali imeendelea kuweka kipaumbele suala la kuboresha sekta ya elimu ikiwa Ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na ajira mpya kwa walimu