Dodoma FM

Nala bado yakabiliwa na changamoto ya maji

4 April 2024, 5:27 pm

Serikali kupitia Wizara ya Maji na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imewekeza kiasi cha shilingi bilioni 9.14 ikiwa ni hatua za haraka za kutatua changamoto ya maji.Picha na George John.

Serikali kupitia Wizara ya Maji na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imewekeza kiasi cha shilingi bilioni 9.14 ikiwa ni hatua za haraka na muda mfupi zilizofanyika za kutatua changamoto ya maji pamoja na uchimbaji na uendelezaji wa visima 32 sehemu mbalimbali za huduma.

Na Mindi Joseph.
Pamoja na jitihada za Duwasa kuchimba visima vya Maji katika Kata ya Nala bado changamto ya maji imeendelea kuikabili kata hiyo.

Ahadi iliyotolewa na Duwasa kwa wananchi ya kutatua changamoto ya maji ni ujenzi wa tenki la maji ambalo litapokea maji kutoka kata ya Zuzu lakini hadi sasa ujenzi huo haujafanyika.

Diwani wa kata ya Nala Herumani Masila amebainisha hayo wakati wa mahojiano na Dodoma TV.

Sauti ya Diwani wa kata ya Nala Herumani Masila ,
Picha ni eneo la Nzuguni ambapo huduma ya maji inapatikana tofauti na awali.Picha na George John.

Kufuatia changamoto hiyo tumezungumza na Mhandisi James Rioba ambaye ni Mhandisi wa maji DUWASA anasema kwa Dodoma hakuna eneo litakalo salia na changamoto ya maji kwani Nala na michese zimechimbiwa visima vya maji Tayari.

Sauti ya Mhandisi James Rioba.

.