Dodoma FM

Rais kuhudhuria siku ya mashujaa (Karume day) Zanzibar

7 April 2021, 5:42 am

Na; Mariam Kasawa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan jana tarehe 06 Aprili, 2021 aliwasili Zanzibar akitokea Jijini Dar es Salaam ambapo atahudhuria maadhimisho ya Siku ya Mashujaa (Karume Day) itakayofanyika katika Ofisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume, Mhe. Rais Samia alipokelewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na baadaye alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar jana tarehe 06Aprili 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Hussein Ali Mwinyi mara baada ya kuwasili Zanzibar .