Dodoma FM

Vilindoni yakabiliwa na upungufu wa matundu ya vyoo

9 October 2023, 8:16 pm

Picha ni vyoo hivyo vilivyopo shuleni hapo ambavyo havikidhi matumizi ya wanafunzi kutokana na kuwa vichache. Picha na George John.

Shule zinapaswa pamoja na mambo mengine kuwa na vyoo bora na vya kutosha kwa walimu na wanafunzi.

Na Mindi Joseph.

Shule ya Msingi Vilindoni inakabiliwa na uhaba wa matundu ya vyoo 15.

Shule hiyo inajumla ya matundu 9 ya vyoo ya wasichana 5 na wavulana 4 kama anavyozungumza Mwalim Mkuu wa shule Hiyo Dorotea Mdushi

Sauti ya Mwalim Mkuu wa shule Hiyo Dorotea Mdushi
Picha ni Diwani wa kata ya Mbabala Bi. Paskazia Mayala akiongea na Dodoma Tv. Picha na George John.

Diwani wa kata ya Mbabala Paskazia Mayala anasema changamoto ya matundu ya Vyoo ni kwa shule za msingi na sekondari hivyo tayari jitihada zimeanza kufanyika.

Sauti ya Diwani wa kata ya Mbabala Paskazia Mayala .

Kulingana na sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 na sheria ya elimu ya mwaka 2016, pamoja na sheria ya afya msingi ya mwaka 2017 zinaelekeza kuwa shule zinapaswa pamoja na mambo mengine kuwa na vyoo bora na vya kutosha kwa walimu na wanafunzi.