Dodoma FM

Wazazi watakiwa kuzingatia malezi ya watoto

27 December 2023, 5:48 pm

Picha ni Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Bi. Pili Mbaga wakati akizungumza na wadau wa elimu Jijini Dodoma. Picha na Aisha Alim.

kwa upande wake afisa elimu mkoa ameahidi kuyafanyia kazi yale yote waliyojadili katika kikao hicho.

Na Aisha Alim.
Wazazi na walezi wameaswa kuhakikisha watoto wao wanakuwa katika maadili mema kwa kuwaepusha na mambo ambayo hayawezi kuwajenga vyema katika makuzi yao.

Hayo yamesemwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Mbagawakati akizungumza na wadau wa elimu na kusema kuwa wazazi wamejikita zaidi katika utafutiaji wa pesa na kusahau kuzingatia malezi ya watoto wao.

Sauti ya Bi Pili Mbaga.
Picha ni wadau wa elimu Mkoani Dodoma wakiwa katika kikao hicho. Picha na Aisha Alim.

Aidha amesema kuwa suala la mmomonyoko wa maadili limekuwa changamoto kubwa huku chanzo chke kikiwa ni pamoja na kuiga tamaduni kutoka mataifa ya nje.

Sauti ya Bi. Pili Mbaga.

Pamoja na mambo mengine amewapongeza walimu kwa kazi kubwa ya kusimamia maadili ya watoto shuleni.

Sauti ya Bi. Pili Mbaga.