Dodoma FM
Dodoma FM
29 April 2026, 16:25

Aidha wamedai kuwa endapo serikali ikizipatia shule vifaa hivyo vya kufundishia na kujifunzia kutaleta usawa wa Kielimu Kwa makundi yote.
Na Steven Noel.
Wahitimu wa Taalauma ya ualimu Katika chuo cha ualimu Mpwapwa wameiomba serikali kuwa uboreshaji wa mitaala uendane na upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia shuleni.
Wameyasema hayo Katika maafali ya 103 ya chuo cha ualimu Mpwapwa .
Wamesema serikali imekuwa ikijitahidi kufanya Maboresho ya Mitaala ukiwemo mtaala wa amali na Elimu jumuishi ambapo walisema uboreshaji huo hauendani na upatikanaji wa vifaa hivyo Katika shule hasa shule za pembezoni.
Kwa upande wake mgeni rasmi Katika maafali hiyo ambae ni kaimu meneja wa benki ya NMB Kanda ya kati Bi Beatrice Ng’ wasa alisema pamoja na kuwapo Kwa upungufu wa vifaa hivyo lakini Jamii inatakiwa kutambua mchango mkubwa wa serikali ulioufanya Katika sekta ya Elimu Kwa ngazi zote.
Amesema pamoja na serikali kuwekeza nguvu kubwa Katika eilimu pia walimu tarajali hao wajitahidi kulinda Maadili ya ualimu na kubuni kazi za kujingizia kipato kabla hawajapata ajira rasmi.
Chuo cha ualimu Mpwapwa ni miongoni mwa vyuo vikongwe hapa nchini na Katika maafali hiyo ya 103 Jumla ya wahitimu 433 walihitimu ikiwa wahitimu 122 walihitimu ngazi ya stashada ya Elimu maluumu miaka mitatu na wahitimu 131walihitimu ngazi ya stashahada Elimu maluumu miaka miwili.