Dodoma FM
25 May 2026, 16:24

Lengo la mabadiliko haya ni kuboresha ukusanyaji wa mikopo, kupunguza vikundi vya mbamba na kuimarisha maendeleo ya wananchi wadogo wa kiuchumi.
Na Mariam Kasawa.
Mikopo ya asilimia 10 inatolewa na halmashauri kwa vikundi vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu. Halmashauri zinatakiwa kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kutoa mikopo isiyo na riba.
Serikali ya Tanzania imeanzisha mfumo mpya wa utoaji wa mikopo kwa vikundi mbalimbali, ikijikita zaidi kwenye ufanisi na uwazi katika mchakato wa ukopaji.