Dodoma FM

Wakulima wa zabibu walalamikia uhaba wa soko la uhakika

6 June 2023, 5:02 pm

Wakulima wa Zabibu wakiwa wamepaki zabibu kwaajili ya kuuza. Picha na Mindi Joseph.

Na Mindi Joseph.

Wakulima wa zao la zabibu kijiji cha Makag’wa mkoani Dodoma wamesema ukosefu wa soko la uhakika ikiwemo idadi ndogo ya viwanda vya kusindika zabibu kumechangia kurudisha nyuma maendeleo ya wakulima wa zao hilo.

Wakulima hao wameeleza hayo wakati wakizungumza na Taswira ya Habari.

Sauti za wakulima wa Zabibu.
Diwani wa kata ya Makag’wa Solomoni Samwel . Picha na Mindi Joseph.

Diwani wa kata ya Makag’wa Solomoni Samwel anasema kilio cha wakulima wa zao la zabibu kinapaswa kufanyiwa kazi ili uhakika wa soko uwepo.

Sauti ya Diwani wa kata ya Makag’wa .

Soko la zabibu limeendelea kusuasua, hali inayofanya baadhi ya wakulima kukata tamaa na kushindwa kuongeza kasi ya uzalishaji kutokana na gharama wanazokutana nazo, huku wakishindwa kupata soko la uhakika.