Dodoma FM

Wakazi wa Karume waomba kuwekewa alama za vivuko  barabarani

5 September 2023, 4:01 pm

Wananchi hao wameiomba Serikali kupitia uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania  (TANROAD) kuweka Alama za Barabarani  ikiwemo michoro ya Pundamilia.Picha na Mtaa kwa mtaa.

Wananchi wanadai kukosekana kwa alama za barabarani katika eneo hilo kunapelekea baadhi ya watu kuendesha vyombo vya moto kwa kasi na kupelekea ajali za mara kwa mara.

Na Asted Bambora.

Imeelezwa  kuwa ukosefu wa AIama za Barabarani hususani mchoro wa Pundamilia katika Eneo la Kwamudi, Mtaa wa Karume jijini Dodoma ni sababu ya uwepo wa ajali za mara kwa mara katika eneo hilo .

Wakizungumza na Kituo hiki  baadhi ya wananchi wa mtaa wa karume uliopo kata ya Mailimbili jijini Dodoma wameiomba Serikali kupitia uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania  (TANROAD) kuweka Alama za Barabarani  ikiwemo michoro ya Pundamilia,Alama za Matuta   katika Barabara  itokayo Dodoma kuelekea Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ili kupunguza ajali .

Sauti za Wakazi wa mtaa wa Karume.
Picha ni mishari inayo chorwa barabarani kwaajili ya kuwasaidia waenda kwa miguu kuvuka kwa urahisi.Picha na Vijimambo.

Bwn.Hussein Shosho  ni Dereva Bodaboda katika mtaa huo ameomba mamlaka inayohusika  kuweka Alama za Barabarani  kuwasaidia kuweka alama hizo katika eneo la kwa  Mudi  ili kupunguza mwendo kasi wa vyombo vya moto.

Sauti ya Hussen Shosho.

Kwa upande wake , Mwenyekiti wa Mtaa wa Karume Bw.Matwiga Kyatya  amekiri  kuwepo kwa ajali nyingi katika eneo hilo  huku akitaja chanzo  kuwa ni ukosefu wa Alama za Barabarani .

Sauti ya Bw.Matwiga Kyata.