Watumiaji wa mifumo ya majitaka watakiwa kuwa na utu
1 July 2026, 16:14

Kampeni yake ya “Usafi wa Mazingira ni Utu” inayo tekelezwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira DUWASA jijini Dodoma inaendelea kutoa Elimu kwa Umma na kuwataka watumiaji wa mifumo ya majitaka kuwa wastaarabu.
Na Mariam Kasawa.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kupitia Kampeni yake ya “Usafi wa Mazingira ni Utu” imeendelea kuwakumbusha na kuwataka watumiaji wa mifumo ya maji taka kujenga tabia ya matumizi sahihi ya mifumo hiyo ili kuepusha kero kwa wananchi wengine.
Mamlaka hiyo Katika Oparesheni zake za kila siku imebaini katika baadhi ya maeneo, hasa ya Royal kwa wachoma kuku, Machinga Complex, Bahi road na katika baadhi ya maeneo yenye Hotel na Migahawa mikubwa wamekuwa chanzo cha matumizi yasiyo sahihi ya mifumo ya majitaka hivyo kusababisha kero kwa wananchi wanaozunguka maeneo yao pamoja na wapita njia.
Aidha wamesema uharibifu wa mifumo ya maji taka katika maeneo hayo unatokana na kutumbukiza taka ngumu kwenye chemba za majitaka, kutumbukiza vyooni nguo, taulo za kike, chupa za maji na mafuta na kwa wale wa Hoteli na Migahawa baadhi yao wanamwaga mafuta ya kupikia na mabaki makubwa ya vitoweo hasa samaki, kuku na mifupa ya nyama jambo linalopelekea kuziba kwa mifumo hiyo na na kusababisha kero kwa wananchi na gharama kwa Mamlaka ya kurekebisha kila mara mifumo hiyo

Kampeni yake ya “Usafi wa Mazingira ni Utu” inayo tekelezwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira DUWASA jijini Dodoma inaendelea kutoa Elimu kwa Umma na kuwataka watumiaji wa mifumo ya majitaka kuwa wastaarabu na wao waelimishane kwenye kaya zao na wafanyakazi wao katika maeneo yao ya kazi juu ya matumizi sahihi ya miundombinu ya majitaka ili kuiepusha jamii na magonjwa ya mlipuko.