Dodoma FM

Zaidi ya milioni 300 zakamilisha ujenzi shule ya msingi Swaswa

29 August 2023, 4:16 pm

Picha ni mwonekano wa shule hiyo mpya iliyojengwa kupitia mradi wa Boost. Picha na George John.

Mtaa wa Swaswa una wakazi wapatao 10,941 huku shauku ya wanafunzi na wazazi ikiwa ni kuona shule hiyo inaanza kutumika baada ya kukamilika kwa ujenzi, usajili na miundombinu mingine.

Na Mindi Joseph.

Zaidi ya shilingi milioni 300 zimetumika katika ujenzi wa shule ya msingi Swaswa kupitia Mradi wa Boost.

Mtaa wa Saswa haukuwahi kuwa na shule huku wanafunzi wakilazimika kwenda kusoma shule ya msingi Ipagala pamoja na Mlimwa C.

Baadhi ya wakazi wa Swaswa wakiongea na Dodoma Tv . Picha na George John.

Baadhi ya wananchi wamepongeza kukamilika kwa ujenzi huo kwani utaondoa changamoto ya watoto kuchelewa shuleni na kutembea umbali mrefu.

Sauti za Wananchi.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Swaswa Charles Nyuma anasema Mtaa huo wenye wakazi wengi haukuwahi kuwa na shule.

Sauti ya Bw. Charles Nyuma .