Dodoma FM

Serikali kuendelea na utaratibu wa kujenga na kukarabati vyuo vya watu wenye ulemavu

28 September 2021, 1:49 pm

Na; Mariam Matundu.

Serikali imesema inaendelea na utaratibu wa kujenga na kukarabati vyuo vya watu wenye ulemavu  lengo ni kuwasaidia kupata elimu ili wajikwamue kiuchumi.
 
Kauli hiyo imetolewa hii leo Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu Ummy Nderiananga mara baada ya kupokea msaada wa baskeli za watu wenye ulemavu 55 na Fimbo za wasioona 50 kutoka Taasisi ya ASA Microfinance Limited na kusema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kila mtanzania anapata haki yake bila vikwazo.
 
Amesema Kwasasa wizara inaratibu kwa kasi ujenzi wa vyuo vya watu wenye ulemavu na ufufuaji wa Vyuo  ambavyo vipo ili walemavu waweze kupata ujuzi huku akiwaomba wadau kushirikiana na serikali katika kuwawezesha walemavu.
 
 

Kwa upande wake Afisa sheria wa Taasisi ya ASA Microfinance Limited,Zephania Paulo  amesema  wametoa  msaada huo wenye thamani ya Sh. milion 13nukta 9 na kwamba wataendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha wanaisaidia jamii kuepukana na umaskini.

Nao watu wenye ulemavu ambao wamepatiwa msada huo wameishukuru Serikali pamoja na Taasisi ya ASA kwakuwapatia msaada huo.