Dodoma FM

Rais Samia kuhudhuria kumbukizi ya miaka 40 ya hayati Sokoine

28 March 2024, 7:07 pm

MSEMAJI  wa familia ya Hayati Sokoine Bw. Lembris Kipuyo,akizungumza  na waandishi wa habari leo Machi 28,2024 jijini Dodoma.Picha na Michuzi Blog.

Hayati Sokoine alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika vipindi viwili wakati wa uongozi wa awamu ya kwanza.

Na Selemani Kodima.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kumbukizi ya miaka 40 ya Hayati Edward Moringe Sokoine aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayo yameelezwa na msemaji wa familia ya hayati Edward Sokoine, Bw. Lembris Kipuyo alipokutana na kuzungumza na waandishi wa habari leo Machi 28, 2024 jijini Dodoma, kwa lengo la kuwaalika watanzania wote kwenye ibada maalum ya kumbukizi ya miaka 40 ya Hayati Edward Moringe Sokoine.

Amesema ibada hiyo iliyoandaliwa na familia ikishirikiana na Taasisi ya Hayati Edward Moringe Sokoine itafanyika siku ya Ijumaa Aprili 12, 2024, saa 3:00 asubuhi katika Kijiji cha Enguik, Monduli Juu mkoani Arusha.

Amesema lengo kubwa la kuanzishwa kwa Taasisi ya Hayati Edward Moringe Sokoine ni kuenzi mema aliyoyafanya kwani aliacha alama kubwa ambayo taifa linamkumbuka hadi leo na kueleza kuwa taasisi hiyo imejikita katika masuala ya elimu, kilimo, hifadhi ya mazingira, vyanzo vya maji pamoja na afya.

Sauti ya Bw.Lembris Kipuyo.