Balozi wa shina afariki baada ya majaribio mawili ya kujiua
9 September 2024, 7:52 pm
Na Nazael Mkude. Balozi wa Shina namba 10 anayejulikana kwa jina la John Mathayo Mkutani Mkazi wa Mtaa wa Miganga kata ya Mkonze jijini Dodoma amekutwa amejinyonga hadi kufa katika moja ya shamba la jirani na makazi yake mwishoni mwa wiki jana.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Miganga Kata ya Mkonze Dodoma Bwm Rudovick Christan Chogwe alifika eneo la tukio baada ya kutaarifiwa mawasiliano ya simu toka kwa kwa Mwenyekiti wa Mtaa Chidachi aliyejulikana kwa jina moja Bwn Papaa kuwa katika mtaa wake kuna tukio la mtu amejinyonga.
Mke wa marehemu Bi Agnes Mathayo ambaye ameishi na marehemu toka mwaka 1993 kwa kuda wote huo marehemu hakuwa na tatizo lolote la kiafya . Katika siku za hivi karibuni amesemea kuwa kabla ya kufikwa na umauti Bwn. John Mathayo Mkutani alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kuchanganyikiwa.