Dodoma FM

Dodoma kunufaika na kipimo cha akili unde kwa wajawazito

30 April 2026, 17:50

Kikao hicho,kimelenga kutambulisha na kujadili juu ya mradi mpya wa utafiti.Picha na Mkoa wa Dodoma.

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa muongozo, kila mwanamke mjamzito anapaswa kupata huduma hiyo ya utrasound kabla ya wiki 24 ya ujauzito, hivyo kwa uwepo wa huduma hiyo ya Utrasound watawezesha upatikanaji mzuri, na kwa wakati kama inavyoelekezwa kwenye miongozo.

Na Mariam Kasawa.

Mganga mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk.Thomas Rutachunzibwa amekutana na kufanya mazungumzo na Wataalamu wa Utafiti kutoka chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Kikao hicho,kimelenga kutambulisha na kujadili juu ya mradi mpya wa utafiti ambao utaanzishwa Katika Halmashauri zote 08 za Mkoa wa Dodoma.

Aidha lengo mahususi la mradi huo ni kuangalia uwezekano wa kutumia Ultra sound ya Akili Unde (AI) katika utoaji huduma za afya kwa wanawake wajawazito. Mradi huo utatekelezwa katika vituo 40 ikiwemo zahanati na vituo vya afya ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na kusaidia utoaji wa huduma bora zaidi kwa Wajawazito.

Kwa upande wake Mhadhiri Mwandamizi na Mtafiti Mkuu Dkt.Leonard Katambula amesema wanaongeza wigo mpana kwa wanawake kwa upatikanaji wa huduma bora hasa ya ultrasound kwa Wajawazito mara tu wanapohudhuria kliniki. Hii itaongeza muitikio wa kuhudhuria kliniki kwa Wajawazito na utambuzi wa changamoto za ujauzito mapema.

Sauti ya Dk.Thomas Rutachunzibwa.