Dodoma FM

Ucsaf yafadhili wanafunzi Wasichana katika Fani ya Sayansi

8 December 2023, 5:10 pm

Zoezi la utiaji saini wa Mikataba ya Ufadhili wa masomo kwa wasichana ,Katikati ni Mtendaji Mkuu wa Ucsaf Justina Mashiba .Picha na Mariam Matundu

Kwa mwaka wa fedha 2023/2024 UCSAF inawafadhili wanafunzi wasichana 6 kutoka chuo kikuu cha Dodoma ,Chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha Mbeya MUST na Taasisi ya teknolojia Dar es salaam DIT ambapo katika kipindi chote cha masomo ya wanafunzi hao UCSAF itagharamia gharama zote.

Na Mariam Matundu.

Wanafunzi 6 wasichana kutoka chuo kikuu cha Dodoma,MUST na DIT wanaosoma shahada ya kwanza ya sayansi inayohusiana na mawasiliano wamepata ufadhili wa kusomeshwa na mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF kwa kipindi chote cha masomo yao.

Akizungumza wakati wa utiaji saini mikataba ya ufadhili huo kati ya UCSAF na chuo kikuu cha Dodoma pamoja na wanafunzi waliopata nafasi hiyo mtendaji mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote Justina Mashiba amesema kuwa ufadhili huo unahusisha gharama zote za masomo,

Sauti ya Mtendaji Mkuu wa Ucsaf Bi,Justina Mashiba

Akimwakilisha makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma, Dkt Florence Rashidi kutoka chuoni hapo amesema kuwa ufadhili huo utaongeza chachu ya wasichana kupenda kozi za sayansi kwani kwa sasa idadi yao ni ndogo huku kiongozi wa serikali ya wanafunzi UDOM akisisita waliopata nafasi hiyo kuitendea haki.

Sauti ya Dkt Florence Rashid na Kiongozi wa Udoso

Nao wanafunzi waliopata nafasi kutoka chuo kikuu cha Dodoma Rebeka Mwakyembe na Mariam Fweda wamesema kuwa watahakikisha wanazingatia masomo ili kuendelea kukidhi vigezo vya ufadhili na kutimiza ndoto zao.

Sauti za Wanafunzi waliopata Ufadhili Udom