Dodoma FM

Wadau waitaka serikali kudhibiti usafirishaji wa binadamu

1 August 2023, 2:51 pm

Asilimia 50 ya watu wanaosafirishwa wanatumikishwa kingono ilhali asilimia 38 ni utumikishwaji kwenye ajira mbalimbali.

Na Fred Cheti.

Wadau mbalimbali wa masuala ya kupinga usafirishaji haramu wa binadamu wameitaka serikali kuweka mikakati madhubuti ya kudhibiti usafirishaji wa binadamu hapa nchini.

Wameyasema hayo jijini Dodoma kwenye maadhimisho ya siku ya kupinga usafirishaji haramu wa binadamu kwa 2023 yaliyoanza kwa maandamano kupita sehemu mabalimbali za jiji la Dodoma yakiwa na kauli mbiu isemayo “Komesha Usafirishaji Haramu wa Binadamu”.

Sauti za wadau.
Maandamano yaliyofanyika sehemu mabalimbali za jiji la Dodoma hapo jana yakiwa na kauli mbiu isemayo “Komesha Usafirishaji Haramu wa Binadamu”. Picha na Fred Cheti.

Kwa upande wake Bwana Ponsiano Kirobombo ambae ni afisa uchunguzi kutoka Tume ya Haki za Binadamu amesema tume hiyo itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa kupinga usafirishaji haramu wa binadamu ili kukomesha vitendo hivyo.

Sauti ya Afisa uchunguzi kutoka tume ya haki za binadamu .

Tarehe 31 Julai kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu usafirishaji haramu wa binadamu duniani ambapo Umoja wa Mataifa unasema mwaka 2018 watu 50,000 walibainika katika nchi 148 kuwa wamesafirishwa kiharamu.