Dodoma FM

Kushuka kwa bei ya mafuta ya kupikia kwaleta neema kwa wananchi

17 May 2023, 4:19 pm

Picha ni moja ya Duka la mafuta ya Alizeti lilipo mtaa wa Majengo Jijini Dodoma. Picha na Thadei Tesha.

Kwa mujibu wa wafanyabiashara hao wanasema kuwa kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo kumechangiwa pia na msimu wa mavuno hususani zao la alizeti.

Na Thadei Tesha.

Kushuka kwa bei ya mafuta ya kupikia kumetajwa kuleta unafuu kwa wananchi pamoja na wafanyabiashara wa chakula Jijini Dodoma.

Dodoma Tv imefanya mahojiano na baadhi ya wananchi jijini Dodoma ambapo wamesema kuwa kufuatia kuwepo kwa msimu wa mavuno kwa kipimdi hiki kumepelekea bei ya bidhaa ya mafuta kushuka na hivy kuleta unafuu kwa wananchi.

Sauti za Wananchi
Baadhi ya wananchi wanasema kama bei pia ya vyakula itashuka italeta unafuu wa maisha. Picha na Thadei Tesha.

Aidha wameongeza kuwa endapo pia bidhaa za vyakula zitashuka itasaidia kupunguza makali ya uwepo wa hali ngumu ya maisha.

Baadhi ya wafanyabiashara wa mafuta ya kupikia jijini hapa wanaelezea hali halisi ya bei ya bidhaa hiyo sokoni kwa hivi sasa.

Sauti za wauzaji wa mafuta.