Dodoma FM

Rais Samia awataka wananchi kujikinga na uviko 19 kwa kupata chanjo

18 October 2021, 12:59 pm

Na; Fred Cheti.

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hasani amewataka watanzania kujikinga na uviko 19 kwa kupata chanjo ili kuipunguzia serikali gharama zitakazotokana na matibabu ya ugonjwa huo.

Rais Samia ameyasema hayo leo octoba 18 jijini Arusha wakati akizindua miradi mbalimbali ikewemo mradi wa maji ambapo amesema kuwa watu wakichanja wataepukana na maradhi hayo pia wataipunguzia serikali gharama nyingine ikiwemo ujenzi wa viwanda vya kuzalisha hewa tiba pamoja na ununuzi wa mitambo ya hewa endapo watapata maradhi hayo.

Aidha Rais Samia amesema kuwa Serikali itaendelea kutekeleza miradi mbalimbali katika awamu hii ya sita ili kuhakikisha wananchi wananufaika ambapo leo amezindua kiwanda cha nyama cha Elius food Overseas LTD pamoja na mradi mkubwa wa maji wilayani Longido wenye thamani ya shilingi bilioni 15.7 ambao unatarajiwa kuwanufanisha wananchi wa wilaya hiyo na vitongoji vyake .

Kwa upande wake waziri wa viwanda na biashara Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa wanaendelea kutekeleza maelekezo ya Mh Rais ikiwemo kuanzisha Mitaa ya viwanda (industrial party) katika kila mkoa na almashauri ambapo mpaka sasa amasema jumla ya viwanda 80,969 vimeshajengwa nchini ikiwemo viwanda vidogo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameendelea na ziara yake Mkoani Arusha ambapo leo ametembelea wilaya Longindo na kufanya uzinduzi wa kiwanda cha nyama pamoja na mradi mkubwa wa maji wilayani humo wenye thamani ya shilingi bilioni 15.7 za kitanzania.