Dodoma FM

WAVIU watakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya ARV

21 September 2023, 2:37 pm

Picha ni mtaalamu wa dawa kutoka jijini Dodoma Dk Mathew Reuben.Picha na Katende Kandolo.

Kwa mujibu wa wataalam wa afya wanashauri kwamba ni vema wananchi kuhakikisha wanapima afya hususani maambukizi ya virusi vya ukimwi ili waweze kujitambua na kutumia dawa kwa usahihi.

Na Katende Kandolo.

Watu walioathirika na maambukizi ya virusi vya UKIMWI wametakiwa kutumia kwa usahihi dawa za kufubaza makali ya virusi hivyo ili dawa ziweze kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.

Dodoma Tv imefanya mahojiano na mtaalam wa dawa kutoka hospitali ya huduma iliyopo jijini Dodoma Dkt. Mathew Reuben ambapo amezungumzia madhara yatokanayo na kukatisha matumizi ya dawa za ARV.

Amesema endapo mtu akipuuza au asipotumia kwa usahihi dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi inaweza kumsababishia athari katika afya yake kama anavyoeleza.

Sauti ya Dk Mathew Reuben.
Picha ni aina mbalimbali za dawa.Picha na Katende Kandolo.

Aidha amewataka wananchi kuwa na utaratibu wa kupima mara kwa mara maambukizi ya virusi vya ukimwi ili waweze kujitambua na kupata matibabu kwa urahisi.

Sauti ya Dk Mathew Reuben.