Wanaume watakiwa kusimama katika nafasi zao katika malezi
17 July 2026, 16:32

Wananchi wanaamini kuwa nafasi ya mwanamume katika malezi ni kubwa kwa sababu watoto hujifunza zaidi kupitia matendo kuliko maneno.
Na Daniel Njau.
Wanaume wametakiwa kusimama katika nafasi zao ili kujenga jamii yenye maaadili na kujituma.
Baba anayewajibika kwa familia yake, anayeheshimu mama wa watoto, anayefanya kazi kwa bidii na kushiriki katika malezi ya kila siku huwajengea watoto maadili ya nidhamu, uwajibikaji na kujituma.
Kwa upande wake, mtaalamu wa malezi na maendeleo ya jamii Bw Fortidas Bakuzi anaeleza kuwa mwanaume bora huanza kujengwa tangu akiwa mtoto kupitia malezi yenye upendo Madili na mazingira salama.
Wanasisitiza kuwa watoto wa kiume wanapaswa kulelewa katika mazingira yanayowafundisha kuwajibika, kuheshimu wengine, kufanya kazi kwa bidii na kutatua changamoto kwa busara.
Aidha, wananchi wanasema dhana ya kwamba malezi ni jukumu la mama pekee imepitwa na wakati. Wanaeleza kuwa ushiriki wa baba katika malezi huimarisha mahusiano ya kifamilia na kuongeza kujiamini kwa watoto.