Dodoma FM

Kaizer Chiefs kucheza na Yanga kesho

21 July 2023, 4:48 pm

Kikosi cha Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kimewasili Alfajiri ya leo kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji wao. Picha na Binzubeiry.

Karibu upate habari za michezo kutoka hapa Nchi Tanzani zikisimuliwa kwako na mwana michezo wetu Rabiamen Shoo.

Na Rabiamen Shoo.

Kikosi cha Kaizer chiefs ‘Amakhosi’ kimetua Tanzania kwa ajili ya Mchezo wa Kirafiki dhidi ya Yanga kwenye Kilele cha Wiki ya Mwananchi.

Baadhi ya Viongozi wamezungumza kuhusu Mchezo huo na kueleza kuwa hawana hofu na Yanga ni kipimo sahihi kwao.

Aidha wamepongeza Usajili wa Skudu na kutaja sifa zake kwani ni Mchezaji wanae mfahamu.

ALLY KAMWE

=========================================

Baada ya kupoteza mchezo wake wa pili dhidi ya Esperance de Tunis ya nchini Tunisia, Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssoupha Dabo, ametamba kuwa ataendelea kukijenga kikosi kuikabili timu ya US Monastir.

Akizungumza baada ya mpambano dhidi ya Esperance de Tunis, Kocha Dabo alisema lengo lake ni kucheza mechi ngumu, kuhakikisha anaangalia uwezo wa kila mchezaji wake

Dabo amesema kesho Jumamosi (Julai 22) watacheza mchezo mwingine dhidi Monastir, lengo kubwa la kucheza mechi hizo ngumu ni kukijenga kikosi chake kuweza kuwa imara kwa ajili ya mashindano ya msimu ujao.

Hata hivyo, Afisa Habari wa Azam FC, Hashim lbwe amesema timu yao inaendelea na maandalizi kwa ajili ya msimu ujao na watahakikisha wanarejea wakiwa na makali zaidi.

Amesema kocha wao, ametaka mechi za kirafiki kucheza na timu ngumu ili wachezaji wake wapate uzoefu pale mashindano yatakapoanza.

Azam FC iliondoka nchini Julai 9, mwaka huu, inatarajiwa kurejea nchini Julai 30, mwaka huu.

lkirejea nchini, timu hiyo itakuwa na kibarua kizito dhidi ya Young Africans katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii utakaochezwa Agosti 9, mwaka huu katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

===============================================

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Fadhill Majiha amesema yupo tayari kupanda ulingoni kuzichapa na Tony Rashidi, endapo atatokea promota wa kuandaa pambano hilo.

Majiha mwenye umri wa miaka 29, anashikilia nafasi ya pili katika uzani wa Super Bantam wakati Rashid anashikila nafasi ya kwanza katika uzani huo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Majiha amesema kama itatokea ofa yupo tayari kuzichapa na Rashidi kwa kuwa ni bondia mzuni mwenye kuufahamu mchezo huo.

Kocha wa Rashid Amos Nkondo ‘Amoma’, amesema pia bondia wake yupo tayari kupanda ulingoni na Majiha kama atapewa ofa nono.

Promota wa ngumi za kulipwa nchini, Saada Kasonso, amesema kuwa, yupo tayari kuandaa pambano la mabondia hao ili kumaliza tambo zinazoendelea mitaani.

=======================================

Klabu ya Ihefu FC imeendelea kujiweka sawa baada ya kukamilisha usajili wa kipa Hussein Masalanga na beki wa kushoto, Mpoki Mwakinyuke, ambao msimu uliopita walikuwa wakiichezea Ruvu Shooting, pamoja na Geofrey Manyasi aliyekuwa Geita Gold.

Masalanga na Mwakinyuke wamejiunga na timu hiyo wakitokea Ruvu Shooting baada ya kushuka daraja, huku Manyasi akimaliza mkataba wake ndani ya Geita Gold.

Chanzo kutoka eneo ambalo Ihefu FC imeweka kambi kimedokeza kwamba wachezaji hao tayari wameshajiunga na timu, huku wakisubiri kujiunga na wengine kwa ajili ya kuanza ratiba ya maandalizi ya msimu mpya.

Nje ya wachezaji hao, mwingine ambaye anatajwa kwamba ameshamalizana na Ihefu FC ni beki wa kushoto, Issa Rashid Baba Ubaya’ aliyekuwa Mtibwa Sugar na tayari ameshaaga kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

Wakati huo huo, Ihefu FC imeondokewa na wachezaji wake Nico Wadada, Yahya Mbegu na Andrew Simchimba.