Dodoma FM

Familia zatakiwa kuzingatia lishe bora Bahi

30 June 2023, 5:34 pm

Shaushi Amiri Kaimu Afisa Lishe wilayani Bahi akitoa elimu kwa wakazi wa Nagulo Bahi. Picha na Mariam Kasawa.

Ulaji unaofaa kwa kuzingatia makundi matano ya vyakula unajenga kinga ya mwili na kukabiliana na maambukizi ya magonjwa mbalimbali.

Na Mindi Joseph.

Jamii imehimizwa kuendelea kuzingatia mlo kamili ikiwemo makundi matano ya chakula ili kujenga familia zenye afya bora.

Savera John ni mratibu wa huduma za jamii idara ya afya halmashauri ya wilaya ya Bahi anasema jamii bado ina uelewa mdogo wa makundi matano ya chakula.

Akitoa elimu ya lishe kwa ngazi ya Familia katika kijiji cha Nagulo Bahi amesema Changamoto iliyopo kwa jamii ni lishe hafifu kwani familia nyingi hazizingatii makundi matano ya chakula wakati wa kuandaa mlo wa familia.

Sauti ya mratibu wa huduma za jamii idara ya afya halmashauri ya wilaya ya Bahi.
Akina baba katika kijiji cha Nagulo Bahi wakisikiliza elimu ya Lishe. Picha na Mariam Kasawa.

Shaushi Amiri Kaimu afisa Lishe amesema kila kaya inapaswa kuhakikisha inazingatia makundi hayo matano ya chakula.

Sauti ya Kaimu afisa Lishe.