Dodoma FM

Halmashauri zatakiwa kuanza ujenzi miradi ya Afya na Elimu

16 February 2024, 5:13 pm

Picha ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh. Rosemery Senyamule akiongea katika ziara hiyo. Picha na Yussuph Hassan.

Katika shule ya Msingi Makulu, mkuu wa mkoa amekagua mradi wa ujenzi wa vyumba Vitano vya madarasa, ofisi 2 za walimu uliogharimu kiasi cha Shilingi Milioni 100 na ujenzi wa matundu ya vyoo 12 kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wasichana na wavulana pamoja na vyoo vya walimu walimu kwa gharama ya shilingi Milioni 204, fedha kutoka Serikali kuu.

Na Mariam Kasawa.

Halmashauri za Wilaya Jijini Dodoma zimetakiwa kuhakikisha zinaaza ujenzi katika fedha zilizoigia mwezi Disemba kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya elimu na afya.

Akizungumza katika ziara ya kukagua miradi ya kimaendeleo kwenye shule ya msingi Makulu pamoja na Hospital ya Wilaya ya Dodoma Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemery Senyamule amezitaka halmashauri kufanya utekelezaji huo haraka.

Sauti ya Mh. Rosemery Senyamule.
Picha ni Ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa katika shule ya msingi Makulu.Picha na Yussuph Hassan.

kwa upande mkuu wa wilaya ya Dodoma Alhaji Jabir Shekimweri amesema kuwa maagizo hayo wameanza kuyafanyia kazi.

Sauti ya Alhaji Jabir Shekimweri .

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma Dk.Andrew Method amesema Halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi Bilioni 1.5 ambazo zinajenga Jengo la Mama na mtoto, Maabara na Idara ya Magonjwa ya nje.

Sauti ya Dk.Andrew Method .