Dodoma FM

Viongozi kanisa katoliki waaswa kudumisha amani, baraka

14 June 2023, 12:10 pm

Viongozi wa kanisa kutoka parokia mbalimbali jimbo kuu katoliki Dodoma wakifuatilia mafunzo hayo. Picha na Bernad Magawa.

Viongozi wamekumbushwa kuwa na mshikamo ili kuepusha migongano mbalimbali isiyokuwa ya lazima.

Na Bernad Magawa.

Viongozi wa kanisa jimbo kuu katoliki Dodoma wameaswa kuwa wasikilizaji wazuri wa shida za wale wanaowaongoza huku wakikumbushwa kufanya utafiti wa kina kabla wa kutolea maamuzi katika mambo mbalimbali ili kuleta amani na baraka katika kanisa na jamii kwa ujumla.

Akitoa mafunzo ya uongozi yaliyofanyika katika ukumbi wa Roma Complex kwa mapadri na viongozi halmashauri za walei kutoka parokia zote za jimbo kuu katoliki Dodoma, mkufunzi wa semina hiyo Dkt. Tumaini Matokeo amesema uongozi ni dhamana ambayo ikitumiwa vibaya inaweza kuharibu kabisa furaha ya unaowaongoza.

Sauti ya Dkt Tumaini Matokeo – Mkufunzi Dkt.

Dkt. Tumaini ameongeza kuwa, sifa ya kiongozi bora ni kutokulalamika, kutokata tamaa kirahisi, pia amewaasa viongozi kutoyadharau mawazo ya watu wengine kwani kuna wakati Mungu anaweza kutuma ujumbe wake kupitia watu wa kawaida.

Naye mwenyekiti wa halmashauri ya walei jimbo kuu katoliki Dodoma Joseph Kasiga akizungumza katika mafunzo hayo amewasihi viongozi kuzingatia vema kanuni za uongozi huku wakiheshimu mipaka ya kila mmoja katika kutekeleza majukumu yao .

Akihitimisha Mafunzo hayo ya uongozi, Makamu wa Askofu jimbo kuu katoliki Dodoma Padri Michael Gaula amewakumbusha viongozi kuwa na mshikamano katika kazi ili kuondoa migongano mbalimbali isiyo ya lazima.

Sauti ya Padri Michael Gaula.