Dodoma FM

Ajira katika umri Mdogo zinavyo kwamisha ndoto za mabinti

10 January 2024, 12:04 am

Pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu nchini kukemea ukiukwaji wa haki za binadamu, bado kuna ukiukwaji wa haki za watoto.Picha na Mtanzania.

Kama mwajiri atatoa madai kwamba hakufahamu kwamba mtu aliyemuajiri ni mtoto wakati wa kumpa ajira au kudai kupewa taarifa zisizo sahihi watakua na wajibu wa kuthibitisha kua ilikua sahihi kwa wao au mtu mwingine yeyote mwenye akili timamu kuamini kwamba mtoto huyo alikua na umri wa kuajiriwa.

Na Mwandishi wetu.
Kifungu cha 4 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano ya Kazi ya mwaka, 2004 kinamuelezea mtoto kama mtu mwenye umri chini ya miaka 14 isipokuwa kwa ajira zilizo katika sekta hatarishi, mtoto maana yake ni mtu mwenye umri wa chini ya miaka 18.

Ni kosa kuajiri watoto kinyume na sheria ya kazi inavyosema na adhabu inatolewa chini ya kifungu cha 102 (2) ambacho kinampaHakimu wa Wilaya na Mkazi kutoa adhabu sawa na faini isiyozidi shilingi milioni 5 au kifungo cha mwaka mmoja au vyote faini na kifungo kama mahakama itavyoona inafaa, kutegemea na mazingira ya kesi yenyewe