Dodoma FM

Viongozi watakiwa kusimamia ipasavyo miradi ya serikali

24 March 2023, 1:15 pm

Aliyekuwa katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma B. Fatma Mganga akikabidhi ofisi kwa katibu tawala mpya hapo jana Mh. Ally Gugu. Picha na Alfred Bulahya.

Bi Fatma Mganga amekabidhi ofisi hiyo baada ya kuhamishwa kwenda kuwa Katibu tawala mkoani Singida.

Na Alfred Bulahya.

Aliyekuwa katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bi, Fatma Mganga, amekabidhi ofisi kwa katibu Tawala mpya  Bw. Ally Gugu.

Katika makabidhiano hayo Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amewataka viongozi waliopewa dhamana kuhakikisha wanasimamia ipasavyo miradi inayotolewa na serikali, kwa kuhakikisha pesa iliyotengwa inatumika kukamilisha miradi hiyo kwa wakati ili ianze kutoa huduma kwa wananchi.

Sauti yaMkuu wa mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule,
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule. Picha na Alfred Bulahya.

Kwa upande wake Fatuma Mganga aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma amesema ni wajibu wa viongozi kuweka utu na ubinadamu mbele Katika kutatua changamoto za wananchi.

Sauti ya aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bi. Fatma Mganga.

Katibu tawala mpya wa mkoa wa Dodoma Ally Gugu akibainisha kuwa ataoa ushirikiano katika kuuwezesha mkoa wa Dodoma kuchagia pato la taifa.

Sauti ya Katibu tawala mpya wa mkoa wa Dodoma Ally Gugu