Dodoma FM

Ubovu wa miundombinu Ndachi wachangia kupanda kwa gharama za usafiri

19 March 2024, 6:57 pm

Mtaa huu una wakazi zaidi ya Elfu 6000 na una barabara tatu ambazo zote ni mbovu. Picha na George Joh n.

Kutokana na mvua zinazo endelea kunyesha Jijini Dodoma maeneo mengi yenye barabara za kawaida yamekuwa yakiathirika kwa kiasi kikubwa na hata kukwamisha baadhi ya shughuli za maendeleo.

Na Mindi Joseph.

Ubovu wa miundombinu ya barabara kwa wananchi wa Mtaa wa Ndachi Kata ya Mnadani Jijini Dodoma imechangia kupanda kwa gharama za usafiri.

Mtaa huu wa ndachi una wakazi zaidi ya Elfu 6000 na una barabara tatu ambazo nazo ni mbovu.

Wakazi hao wanaeleza hali halisi ya barabara yao

Sauti za wakazi wa Ndachi.
Picha ni Mkazi wa Ndachi akiongea na Dodoma Tv.Picha na George John.

Mwenyekiti wa mtaa wa Ndachi Justini Lugwalu anasema Barabara zilizopo zote zinajaa maji.

Sauti ya Mwenyekiti wa mtaa wa Ndachi.