Dodoma FM

Stanbic wakabidhi vifaa tiba RRH, BMH na Mirembe

13 May 2026, 17:15

Picha ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh. Rosemery Senyamule akipokea vifaa tiba hivyo.Picha na Mkoa wa Dodoma.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na shuka 300, glovu 150 za upasuaji, sindano 450 na paketi 90 za vifaa vya upasuaji.

Na Mariam Kasawa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amepokea  na kukabidhi vifaa tiba kwa hospital tatu za Mkoa wa Dodoma vyenye thamani ya milion 17 vilivyotolewa na stanbic bank..

Makabidhiano Haayo yamefanyika leo mei 13 katika ofisi ya Mkuu wa mkoa ambapo  hospitali ya Mirembe ,Benjamin mkapa na General wamekabidhiwa vifaa tiba hivyo.

Akizungumza katika hafla hiyo mh Senyamule ameipongeza Stanbic Bank Tanzania kwa kuunga mkono vipaumbele vya sekta ya afya na amezitaka hospitali zilizonufaika kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika ipasavyo.

Sauti ya Mh. Senyamule.

Kwa mujibu wa Meneja wa Tawi la Stanbic Bank Dodoma, Joan Mbise,amesema msaada huo una mchango mkubwa katika huduma kwa wagonjwa na uendeshaji wa shughuli za tiba.

Picha ni mkuu wa Mkoa wa Dodoma mh. Rosemery Senyamule wakati akipokea vifaa tiba hivyo.Picha na Mkoa wa Dodoma.
Sauti ya Joan Mbise.

Baada ya kupokea Vifaa Tiba hivyo Kaimu Mganga mfawidhi wa hospitali  ya rufaa Mkoa Dodoma Dkt.Sarah ludovick na Mwakilishi wa mkurugenzi muuguzi hospitali ya Benjamin mkapa Mayunga mahona Pamoja na Dr Innecent Mwombeki Kaimu Mkurungezi Mtendaji Hospitali ya Taifa ya afya ya Akili wameshukuru kwa msaada huo.

Sauti ya Dkt.Sarah ludovick .