Dodoma FM

Vyuo vya Afya 20 kuchukuliwa hatua kwa kufanya udanganyifu

10 May 2022, 2:02 pm

Na:Mindi Joseph.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof. Abel Makubi ameagiza NACTVATE kuvi chukuliwa hatua Vyuo 20 vya afya vilivyokaguliwa na kufanya udanganyifu ili kulinda viwango vya taaluma ya afya Nchini.

Akizungumza leo Jijini Dodoma katika mkutano wa wakuu wa vyuo vya afya ngazi ya kati Tanzania bara amesema baadhi ya vyuo vimekuwa na walimu ambao hawastahili na kuchangia kuzalisha wahitimu wasio kidhi viwango.

Ameongeza kuwa baadhi ya vyuo vinafanya udanganyifu jambo ambalo halistahili na wizara haitasita kuchukua hatua.

.

Awali akizungumza kwa mwakilishi wa wakuu wa vyuo vya afya ngazi ya kati Daktari Geofrey Mdede ambaye ni Mkuu wa chuo cha songea ameliomba Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi NACTVATE kuzuia mrudikano wa wanafunzi katika vyuo.

.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Twaha Twaha amesema baraza limeshafanya utafiti na baraza limeanza kuchukua hatua kwa vyuo vyenye mrudikano wa wanafunzi.

.

Mkutano wa wakuu wa vyuo wa afya ngazi ya kati Tanzania bara kwa mwaka 2022 unabebwa na kauli mbiu isemayo Huduma bora za afya ni matokeo ya uwepo wa vyuo bora nchini.