Dodoma FM

Mkesha mkubwa kitaifa dua maalum kufanyika Dodoma

23 December 2023, 4:58 pm

Picha ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi mkesha mkubwa kitaifa wa Dua maalum Mchungaji  Godfrey Malasi.Picha na Mariam Kasawa.

Mkesha mkubwa kitaifa dua maalum unatarajiwa kufanyika usiku  December 31 katika viwanja vya Nyerere square jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Na Mariam Kasawa.

Wakazi jijini Dodoma wametakiwa kujitokeza kwenye mkesha mkubwa Kitaifa wa dua maalum utakao fanyika katika viwanja vya Nyerere square jijini Dodoma.

Akiongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa kamati ya maandalizi mkesha mkubwa kitaifa wa Dua maalum Mchungaji  Godfrey Malasi amesema imekuwa desturi ya watanzania kila mwisho wa mwaka kufanya maombi ya kumshukuru Mungu.

Sauti ya Mchungaji  Godfrey Malasi.

Nae Pastor Deborah msimamizi wa timu ya kusifu na kuabudu katika mkesha huo amewataka wakazi wa jijini Dodoma hasa kina mama na vijana kujitokeza kwa wingi katika mkesha huo ili kurudisha shukrani kwa Mungu.

Sauti ya Pastor Deborah .