Dodoma FM

Wanchi Ndachi wakumbwa na sintofahamu Mgogoro wa Ardhi

26 March 2024, 7:42 pm

Picha ni Mtaa wa Ndachi unaopatikana jijini Dodoma .Picha na George John.

Mtaa wa Ndachi umekuwa ukiandamwa na migogoro ya ardhi kwa muda mrefu sasa ambapo kwa mujibu wa mwenyekiti wa Mtaa huo migogoro hiyo bado ina sintofahamu.

Na Mindi Joseph.
Wananchi wa Mtaa wa Ndachi kata ya Mnadani wamesema hawajui hatima yao baada ya kuendelea kushuhudia mgogoro wa ardhi katika maeneo yao.

Changamoto ya ardhi katika mtaa huo imetajwa kuwa sugu tangu mwaka 2014 na Wananchi hao wamezungumza na kituo hiki na kubainisha haya.

Sauti ya Wananchi wa Mtaa wa Ndachi.

Picha ni Mkazi wa Ndachi akiongea na Dodoma Tv juu ya Mgogoro huo wa Ardhi. Picha na George John.

Kwa upande wa mwenyekiti wa Mtaa wa ndachi Jastini Lugwalu anasema walipewa ahadi na waziri wa ardhi kuwa changamoto hii itatatuliwa lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika.

Sauti ya mwenyekiti wa Mtaa wa ndachi.

Ni mwezi mmoja umepita tangu waziri wa Ardhi Nyumba, na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa kusitisha zoezi la uhakiki wa umiliki wa ardhi kwa wananchi wa ndachi kata ya Mnadani na Nkuhungu Jijini Dodoma.

Sauti ya Mh. Jerry Silaa .