Dodoma FM

Wananchi watakiwa kuacha matumizi ya maziwa mabichi

7 November 2023, 4:36 pm

Wananchi wametakiwa kuacha mara moja  utumiaji wa chakula hicho kwani athari zake ni pamoja na tatizo la kifua kikuu na kansa. Picha na Muungwana blog.

Baadhi ya watu wanaokunywa maziwa mabichi huenda wasielewe kikamilifu hatari na huenda wasijue uwezekano wa kupata ugonjwa kutokana na bakteria katika maziwa .

Na Aisha Alim.

Bodi ya maziwa nchini imetoa tahadhari kwa wananchi juu ya kuepuka matumizi ya maziwa mabichi kwani husababisha athari katika afya ya binadamu hususani wanawake wajawazito pamoja na watoto.

Akizungumza na Dodoma tv mteknolojia kutoka Bodi ya Maziwa Tanzania Bi. Neema Mushi amewataka wananchi kufahamu athari na kuacha mara moja  utumiaji wa chakula hicho kwani athari zake ni pamoja na tatizo la kifua kikuu, kansa na magonjwa mengineyo.

Sauti ya Bi. Neema Mushi .

Nilipata wasaa wa kuzungumza na wananchi ambapo wameeleza kuwa na ufahamu mdogo juu ya athari za kutumia maziwa mabichi.

Sauti za wananchi.

Baadhi ya watu wanaokunywa maziwa mabichi huenda wasielewe kikamilifu hatari na huenda wasijue uwezekano wa kupata ugonjwa kutokana na bakteria katika maziwa kwani wajawazito, watoto wadogo na watu wenye kinga dhaifu wapo kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa na madhara yanaweza kuwa makubwa zaidi na wakati mwingine kufikwa na umauti.