Dodoma FM

Muda huu utumike kutoa elimu kwa wakulima

11 February 2021, 2:25 pm

Na,Mariam Matundu,

Dodoma.

Kutokana na kusitishwa kwa maonesho ya Nanenane mwaka huu,wito umetolewa kutumia muda huu kutoa elimu kwa wakulima juu ya umuhimu wa nane nane na nini wanapaswa kufanya katika maonesho hayo ili yawanufaishe kwa miaka ijayo.

Hayo yameelezwa na mtaalamu wa kilimo kutoka taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Japan Tobacco international Ezra Mbugi, alipokuwa akizungumza na Dodoma Fm, ambapo amesema wakulima wengi hawajui kama maonesho hayo ni fursa kwao.

Aidha amesema kusitishwa kwa maonesho hayo kunaweza kuathiri taasisi binafsi na kampuni zinazoyatumia kuuza pembejeo za kilimo, pamoja na wakulima wao kwenda kupata elimu.

Picha ya Maktaba

Baadhi ya wananchi jijini hapa wamesema muda huu ambapo maonesho hayafanyiki utumike kutafakari na kuona ni kwa namna gani maonesho yataleta tija kwa wakulima moja kwa moja.

Hapo jana waziri wa kilimo Prof.Adolf Mkenda alitangaza kusitisha maonesho ya Nanenane mwaka huu na kuagiza pesa zilizokuwa zikitumia katika kuendesha maonesho hayo kuelekezwa katika shughuli za ugani.