Dodoma FM

Wananchi walalamika kutumia maji yasiyo salama

20 March 2023, 3:07 pm

Maji ya mto kizigo ambayo sio safi na salama.Picha na wikipedia

Wakazi walalamika kutumia maji ya mto kizigo ambayo sio safi na salama baaada ya kuharibika kwa mashine ya kusukuma maji.

Na Victor Chigwada.

Wakazi wa kijiji cha Chinugulu wilayani chamwino wamelalamika kutumia maji ya mto kizigo ambayo sio safi na salama baaada ya kuharibika kwa mashine ya kusukuma maji .

Wakielezea adha hiyo wananchi wa Chinugulu wamesema wamekuwa wakitumia maji hayo ya mto ambayo yanawingi wa chumvi hali ambayo sio salama kwa afya zao.

Sauti za wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Sanjeli Njelula ameiomba Serikali kuwasaidia matengenezo ya mashine ya maji pamoja na kuwachimbia kisima cha ziada cha maji .

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Sanjeli Njelula.

Nae Diwani wa Kata ya Chinugulu Bw.Mathiasi Mele amekiri kuharibika kwa mashine ya maji hali inayosababisha wananchi kutumia maji ya mto ambayo kwa upande mwingine yanapatikana umbali mrefu.

Diwani wa Kata ya Chinugulu Bw.Mathiasi Mele.

amesema matumizi ya maji hayo kwa wananchi wa kijiji hicho inahatarisha afya zao licha ya uwepo wa biashara ya maji ambapo wananchi walio wengi wamekuwa wakishindwa kumudu gharama ya ndoo moja ya maji ambayo ni shilingi mia tano