Dodoma FM

Wananchi watakiwa kujitokeza kutoa maoni marekebisho ya katiba

4 January 2024, 9:43 pm

Picha ni Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akiongea na wananchi. Picha na Fred Cheti.

Wadau ,wanasiasa wa vyama vya upinzani pamoja na wananchi wamekua wakitoa maoni tofouti juu marekebisho katika miswada hiyo.

Na Fred Cheti.

Wito umetolewa kwa wananchi kushiriki ipasavyo kutoa maoni na mapendekezo katika Marekebisho ya Muswada wa Sheria za uchaguzi wa Rais,wabunge  na madiwani ya Mwaka 2023 pamoja na  Muswada wa sheria ya Tume ya Taifa ya uchaguzi ya Mwaka 2023.

Hii inajiri baada ya serikali kupitia Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko kuwataka Watanzania kushiriki katika kutoa maoni kuhusu muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2023, Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi wa mwaka 2023 na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2023 ili kuunga mkono jitihada za kujenga Tanzania iliyo bora zaidi katika nyanja zote za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Wito huo umetolewa na Ndugu Twaha Mwaipaya Katibu Mwenezi kutoka Baraza la vijana Chadema (BAVICHA) wakati akifanya mahojiano na Dodoma Tv Kuhusu mapokea yao juu ya jambo hilo.

Sauti ya Katibu mwenezi wa BAVICHA
Picha ni Ndugu Twaha Mwaipaya Katibu Mwenezi kutoka Baraza la vijana Chadema (BAVICHA) wakati akifanya mahojiano na Dodoma Tv .Picha na Fred Cheti.

Aidha Bwana Mwaipaya ameeleza wao kama chama cha upinzani watakavyoshiriki katika kutoa mapendekezo kuhusu marekebisho ya Miswada hiyo.

Wadau ,wanasiasa wa vyama vya upinzani pamoja na wananchi wamekua wakitoa maoni tofouti juu marekebisho katika miswada hiyo ya sheria za uchaguzi wa Rais,wabunge na Madiwani ya mwaka 2023 ,Uchaguzi wa serikali za mitaa  ya mwaka 2023 pamoja Muswada wa sheria ya Tume ya Taifa ya uchaguzi ya mwaka 2023.

Sauti za Wadau,Wanasiasa na Wananchi.