Dodoma FM

Vijana sokoni Majengo waeleza kunufaika na ubebaji mizigo

2 August 2023, 1:36 pm

Vijana hao wanasema licha ya kunufaika na kazi hiyo lakini wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara.Picha na Aisha Shaban.

Wanasema kazi hiyo inawasaidia kujiingizia kipato chao cha kila siku na kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.

Na Aisha Shaban.

Baadhi ya vijana wanaojishughulisha na shughuli ya kubeba mizigo kwa kutumia mikokoteni wameeleza namna shughuli hiyo inavyowasaidia kuendesha shughuli zao na kujikwamua kiuchumi.

Dodoma tv imefika katika soko la Majengo Jijini hapa na kukutana na baadhi ya vijana wanaojishughulisha na shughuli hiyo ambapo kwanza nilianza kwa kuawauliza ni kwa namna gani shughuli hiyo inawasaidia kuendesha maisha yao?

Sauti za vijana wabeba mizigo.

Aidha zipo baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili jambo ambalo linapelekea kutokufanya kazi zao kwa ufanisi uliokusudiwa kama wanavyoeleza baadhi ya changamoto hizo.

Sauti za vijana wabeba mizigo.
Picha ni baadhi ya mikokoteni ya kubebea mizigo ikiwa imepaki sokoni hapo. Picha na Aisha Shaban

Dodoma tv imekutana na mwenyekiti wa waendesha mikokoteni katika eneo la Majengo ambapo alielezea baadhi ya changamoto na fursa za shughuli hiyo kwa waendesha mikokoteni waliopo katika soko la Majengo.

Sauti ya Mwenyekiti.