Dodoma FM

Wakazi Jijini Dodoma waiomba serikali kutatua changamoto ya upandaji wa mafuta

5 May 2022, 1:42 pm

Na; Benard Filbert.

Kutokona na kubadilika kwa mfumo wa maisha kulikosababishwa na kupanda kwa bei ya nishati ya mafuta Duniani wakazi mkoani Dodoma wameiomba serikali kuangalia njia bora ya kutatua changamoto hiyo hali itakayosaidia kuwakwamua wananchi kiuchumi.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wakazi wakati wakizungumza na taswira ya habari kuhusu mwenendo wa maisha ulivyo hivi sasa.

Wakazi hao wamesema kuwa kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta duniani imesababisha maisha kubadilika kwani kila bidhaa imekuwa ikipatikana kwa bei kubwa.

Kadhalika wamesema ni vyema serikali ikaangalia njia bora yakupunguza gharama za maisha ili kunusuru hali ya uchumi kwa wananchi.

CLIP WANANCHI……………01

Usiku wa kuamkia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefanya kikao na baadhi ya viongozi wa serikali na kufanya tathimini ya bei ya mafuta huku akisema Serikali inaendelea kutafuta njia mbadala ambazo zitapunguza gharama ya maisha kwa Watanzania kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.

CLIP WAZIRI MKUU……………02

Kupanda kwa bei ya mafuta duniani ambapo kulikosababishwa na sababu mbalimbali ikiwepo vita kati ya urusi na Ukraine kumeathiri kupanda kwa bei ya bidhaa mbalimbali huku baadhi ya wananchi wakishindwa kumudu bei hizo.