Dodoma FM

Katazo la unyago laungwa mkono na baadhi ya wananchi

21 September 2023, 3:15 pm

Picha ni Rais Samia akiongea na wananchi wa Ruangwa Lindi alipokuwa ziarani mkoani humo. Picha na Ikulu .

Inaelezwa kuwa baadhi ya tamaduni zimekuwa zikiwafundisha mabinti katika unyago mambo ambayo hayastahili.

Na Khadija Ayoub.

Wananchi jijini Dodoma wameonesha kuunga mkono katazo la mh. Rais Samia Suluhu Hassan kuwapelekea watoto wa kike katika unyago kwani ni kuwaonea na kuwanyima haki yao ya msingi ya malezi wanayostahili.

Wananchi hao wakizungumza na kituo hiki wamesema kuwa desturi ya watu kuwapeleka kuwafanyia unyago watoto inaweza kuwasababishia athari kutokana na baadhi ya tamaduni hizo kufundisha mambo yasiyo na maadili.

Sauti za wananchi
Mkazi wa jiji la Dodoma akiongea na Dodoma Tv. Picha na Khadija Ayoub.

Hivi karibuni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa ziarani wilayani Ruangwa mkoani Lindi alikemea tabia ya baadhi ya wazazi kuwapeleka watoto wao kufanyiwa unyago.

Sauti ya Dkt Samia Suluhu.