Dodoma FM
Dodoma FM
4 May 2026, 16:01

Barabara hiyo imekuwa ikizungumziwa bungeni mara kwa mara lakini hakuna utekelezaji wowote ulio fanyika.
Na Steven Noel.
Wananchi wilayani Mpwapwa wasema wamechoshwa na Ahadi za serikali juu ya ukarabati wa barabara .
Kufuatia swali la mbunge wa Jimbo la Mpwapwa bwana Nathani George Malima juu ya ujenzi wa barabara ya Rami kutoka njia panda ya kongwa Hadi Mpwapwa kumeamsha hisia mpya Kwa wakazi hao ambapo wasema kuwa wamechoshwa na Ahadi hizo zisizo na utekelezaji miaka nenda Rudi.
Wakiongea na taswira ya habari wananchi hao wamesema barabara hiyo imekuwa ikizungumziwa bungeni mara kwa mara lakini hakuna utekelezaji wowote ulio fanyika hali inayo wakatisha tamaa.