Dodoma FM

Vijana Dodoma walalamikia kipato kisichokidhi mahitaji yao

10 August 2026, 16:54

Kipato kidogo chatajwa kuwa sababu ya vijana kutokidhi mahitaji yao ya kila siku. Picha na mtandao

Ukosefu wa ajira ni moja ya changamoto kubwa zinazowakabili vijana kote duniani, hasa katika nchi zinazoendelea. Nchi nyingi zinakosa nafasi za ajira za kutosha kutokana na ongezeko kubwa la vijana wanaomaliza masomo kila mwaka Hali hii husababisha vijana wengi kubaki bila ajira, jambo linalowaweka katika hatari ya kukosa mapato na kujikuta wakiathirika kisaikolojia.

Na Godson Mgima.

Baadhi ya vijana Jijini Dodoma wamelalamikia kukabiliwa na changamoto ya ya kipato cha uhakika hali inayo waathiri kupata mahitaji yao ya kila siku.

Taswira ya habari ilizungumza na baadhi ya vijana katika mtaa wa Mwisho wa lami katika kata ya Mnadani ambapo wamesema ukosefu wa ajira unawalazimu kujikita katika shughuli ndogondogo ambazo hazina kipato cha uhakika.

Aidha wamesema changamoto ya ukosefu wa ajira na kipato cha uhakika imekuwa ikiathiri mipango yao ya maisha huku baadhi yao wakilazimika kufanya kazi za muda mfupi na biashara ndogo ndogo huku ujuzi walio nao wakiuweka pembeni ili kupambana na ugumu wa maisha.

Bw Enock Jackson ni Mtaalamu wa uchumi kutoka chuo kikuu cha Iringa yeye anasema changamoto ya kipato kwa vijana ni suala linalo hitaji kupewa kipaumbele na kutatuliwa kwani vijana ni nguvu kazi ya jamii na Taifa .

Amesema mabadiliko ya soko la ajira yana wahitaji vijana kuwa na ujuzi unao endana  na mahitaji ya sasa pamoja na kutafuta njia mbalimbali za kuwekeza katika kujiajiri.

Sauti na Godson Mgima.