Wataalamu wa afya waonya ufanyaji kazi ngumu kwa wajawazito
21 September 2026, 16:55

Si kila shughuli ya mwili ni hatari kwa mama mjamzito, kwani baadhi ya kazi nyepesi zinaweza kusaidia mwili kubaki katika hali ya uchangamfu. Shughuli kama kupika, kuosha vyombo na kazi nyingine nyepesi za nyumbani, huku akisisitiza kuwa mama mjamzito anapaswa kuepuka kazi zinazomchosha kupita kiasi na kufuata ushauri anaoupata kutoka kwa wataalamu wa afya.
Na Daniel Njau.
Wataalamu wa afya wameonya kuwa kufanya kazi ngumu kwa mama wajawazito kunaweza kuhatarisha afya ya mama na mtoto aliye tumboni, huku wakisisitiza umuhimu wa mama wajawazito kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu aina na kiwango cha kazi wanachoweza kufanya.
baadhi ya wananchi wamesema wanawake wajawazito katika jamii hukabiliwa na changamoto za kiafya zinazoweza kuwalazimu kuacha kazi nzito, hasa pale wanapobainika kuwa kazi hizo zinaweza kuhatarisha usalama wao au wa motto aliye tumboni.
Aidha, baadhi ya wazazi wenza wanatajwa kusahau majukumu yao na kuwaacha wanawake wajawazito kufanya kazi nzito kwa lengo la kujikimu kimaisha.
Akizungumza kuhusu suala hilo, mtaalamu wa afya wa magonjwa ya kina mama Bwana Rajabu Yangara, amesema ni muhimu mama mjamzito kuhudhuria kliniki mara kwa mara ili kubaini mapema changamoto zozote za kiafya na kupata ushauri unaofaa kuhusu shughuli anazopaswa kufanya.
Amesema uamuzi wa kuendelea au kuacha kazi fulani unapaswa kuzingatia hali ya afya ya mama na usalama wa mtoto aliye tumboni.