Jamii imetakiwa kutambua haki ya mwanamke kumiliki mali
22 October 2026, 16:38

Miongoni mwa changamoto zinazowakabili wanawake, ikiwemo mila na mitazamo potofu inayowazuia kumiliki mali, hazipaswi kutumika kama sababu ya kuwanyima haki hiyo, hivyo ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa elimu kuhusu haki za wanawake katika umiliki wa ardhi na kuhakikisha wanapata nyaraka halali za kuthibitisha umiliki wao.
Na Daniel njau.
Wananchi wamehimizwa kutumia haki yao ya kisheria kumiliki ardhi na mali nyingine, licha ya changamoto na mila potofu zinazowakabili katika jamii, huku wakisisitizwa kuwa mila na desturi hazipaswi kuwa kikwazo cha wao kupata umiliki halali wa ardhi hasa kwa mwanamke.
Baadhi ya wananchi wamesema baadhi ya mila na desturi hasa vijijijni wana pitia changamoto ya mwanamke kutokumiliki mali hvyo wanakosa haki zao stahiki
Akizungumza kuhusu suala hilo, Mwanasheria Lilian Mmbwana kutoka TAWLA Tawi la Dodoma, amesema kila mtu katika jamii ana haki ya kumiliki ardhi na kupata nyaraka halali za umiliki, ikiwemo hati ya eneo husika. Amesema ni muhimu jamii kutambua kuwa mwanamke ana haki sawa na mwanaume katika kumiliki na kutumia ardhi kwa mujibu wa sheria.