Dodoma FM

Je, unafanya uchunguzi wa afya mara kwa mara bila dalili za Ugonjwa?

24 November 2026, 16:39

Picha ni zoezi la upimaji wa afya likiendelea kwa baadhi ya watu wanaofanya uchunguzi wa afya zao kila baada ya muda fulani. Picha MoETV.

Jamii imeshauriwa kujenga utaratibu wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kubaini mapema viashiria vya magonjwa, kupata matibabu kwa wakati na kuepuka madhara makubwa yanayoweza kujitokeza kutokana na kuchelewa kugundua matatizo ya kiafya.

Na Daniel Njau.

Baadhi ya wananchi, wakiwemo vijana, wamesema uchunguzi wa afya umekuwa na umuhimu mkubwa katika kuwasaidia kufahamu hali zao za kiafya na kuchukua hatua stahiki kwa wakati.

Wananchi hao wamewahimiza wengine kuzingatia utaratibu wa kupima afya hata wanapokuwa hawana dalili za ugonjwa, wakieleza kuwa kufanya hivyo kunasaidia kugundua matatizo ya kiafya katika hatua za awali.

Kwa upande wake, mtaalamu wa afya, Daktari Milton Bernard Kutoka Hospitalo ya Benjamini MKapa, amesema matumizi ya dawa bila kupata ushauri wa wataalamu wa afya yanaweza kuchelewesha utambuzi wa magonjwa na kuongeza hatari ya kupata madhara makubwa.

Daktari Bernard ameshauri jamii kuwa na utaratibu wa kupata ushauri wa kitaalamu kuhusu vipimo vinavyofaa na muda wa kuvifanya, badala ya kusubiri hadi dalili za ugonjwa zijitokeze.

Ripoti ya Daniel Njau.